Washiya waadhimisha Anshura | Habari za Ulimwengu | DW | 30.01.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washiya waadhimisha Anshura

Damu inazidi kumwagika nchini Irak licha ya miito ya kuwepo umoja na amani

Quba la Immam Hussein mjini Kerbala

Quba la Immam Hussein mjini Kerbala

Watu wanane wameuwawa na zaidi ya 30 kujeruhiwa Khanakine,kaskazini mashariki ya Baghdad katika maombolezi ya Anchoura- kuikumbuka siku aliyouwawa Imam Hussein. Waumini zaidi ya milioni moja na nusu wa madhehebu ya shia wameshafika katika mji mtukufu wa Kerbala,umbali wa kilomita 110 kusini mwa Baghdad kuhudhuria kilele cha maombolezi hayo,yaliyoanza siku kumi zilizopita.

Polisi na wanajeshi zaidi ya elfu kumi wanalinda usalama wa mahujaj huko Kerbala ,kusini mwa Baghdad na katika maeneo ya karibu na huko kuepusha pasitokee mashambulio ya umwagaji damu.Polisi wanamsachi kila anaeonyesha dalili mbaya.

Hatua za ulinzi zimezidi makali kufuatia shambulio la leom asubuhi huko Khanakine kaskazini mashariki ya Baghdad unaopakana na Iran.Bomu lililofichwa ndani ya debe la taka limepelekea watu zaidi ya wanene kuuwawa na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa..

Kwa mujibu wa kanali Azad Issa bomu hilo lililengwa dhidi ya jamii ya fayli-wakurd wa madhehebu ya shiya waliokua wakiadhimisha Achoura.Miongoni mwa wahanga wa shambulio hilo ni wanawake na watoto.

Mjini Kerbala kwenyewe ,kilele cha maadhimisho hayo, mahujaj zaidi ya milioni mbili kutoka kila pembe ya dunia wameshazuru Quba la Imam Hussein-mjukuu wa Mtume Mohammad.

Kifo chake katika mapambano ya Kerbala mwaka 680 ndio chanzo cha maombolezi haya yanayofanyika kila mwaka ,mnamo siku ya kumi ya mwezi wa kislam-Muharram,katika kila nchi wanakoishi waislam wa madhehebu ya shia.

Maombolezi hayo ya Anchoura ambapo washiya wanajipiga mpaka wanatokwa na damu, wakijuta kwa kutofanya chochote kunusuru maisha ya Immam wao wa tatu,yameanza tangu January 21 iliyopita na kilele chake kinafikiwa hii leo mjini Kerbala.

Hapo awali mahujaj wa kishia walitoa mwito matumizi ya nguvu yakome na kuimarishwa umoja kati ya waumini wa dini ya kiislam.

“Acheni kumgawa damu,na tuhakikishe Anchoura,maombolezi ya kutubia,inakua siku ya umoja na udugu kati ya wairak-ni miongoni mwa mabango yaliyoandikwa katika maadhimisho ya Achoura mjini Kerbala.

Mchamngu mkuu na amwanasiasa mashuhuri kabisa wa kishiya nchini Irak,Abdel Aziz Hakim nae pia amewatolea mwito wairak waungane .

“Sisi ni wamoja na tunaungana pia katika mapambano yetu dhidi ya magaidi” amesema mkuu huyo wa baraza kuu la mapinduzi ya kiislam nchini Irak.

Wakati huo huo mtu aliyeyatolea mhanga maisha yake amejiripua msikitini huko Dour Mandali,kilomita 80 kaskazini mashariki ya Baghdad na kuangamiza maisha ya waumini 12 na wengine 40 kujeruhiwa.

 • Tarehe 30.01.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CBHU
 • Tarehe 30.01.2007
 • Mwandishi Oummilkheir
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CBHU

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com