1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Wademokrats washindwa kumshawishi rais Bush juu ya muswaada

3 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5E

Wademokrat katika bunge la wawakilishi nchini Marekani wameshindwa kukubaliana na rais Bush juu ya mswaada wa kugharamia vita nchini Iraq baada ya rais bush kuupigia kura ya turufu kuupinga mswaada huo unaotaka wanajeshi wa Marekani waondoke Iraq katika muda maalum.

Rais Bush alikutana na viongozi wa vyama mbali mbali vya kisiasa bungeni katika ikulu yake kujadili hatua ya kuchukuliwa kuhusiana na suala hilo.

Baada ya kikao hicho pande zote zilisema wanahisi kuna umuhimu wa kuupitisha muswaada huo kufikia mwishoni mwa mwezi huu wa Mei. Wakati huo huo kiasi cha wanajeshi 4000 zaidi wa Marekani wamewasili Iraq kwa ajili ya kuongeza nguvu mapambano ya kumaliza mauaji ya kimadhehebu kati ya washia na wasunni.Hapo jana wanajeshi watatu wa Marekani waliuwawa kwenye mashambulio ya mabomu yaliyofanywa mjini Baghdad na zaidi ya watu 70 kuuwawa katika ghasia zilizotokea katika maeneo mbali mbali ya Iraq.