1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Ujerumani itayari kujihusisha kidiplomasia mashariki ya kati ikiwa sera ya Bush itabadilika Iraq

Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amesema Ujerumani itakuwa tayari kuchukua jukumu la kidiploamasia katika mashariki ya kati ikiwa Marekani Marekani itabadili sera yake juu ya Iraq.

Waziri Steinmeir ameyasema hayo akiwa na mazungumzo hapo jana na waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condolezza Rice mjini Washington.

Awali waziri Steinmeir akiwatembelea maseneta alikataa kutoa maoni yake juu ya ripoti kuhusu Iraq akisema kuwa ripoti hiyo haikuwa wazi ni mapendekezo yapi yaliyokubalika kati ya mapendekezo yake 79,kufuatia mjadala mkali nchini Marekani.

Bwana Steinmeier ametumia wasaa huo pia kutetea hatua yake ya kuzuru Syria jumatatu iliyopita kufuatia ukosoaji mkubwa kutoka Israel.

Alisema ziara yake ya Syria ilikuwa muhimu kwani ililenga kuiangalia nchi hiyo endapo itafaa katika kutafuta amani ya mashariki ya kati.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com