1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Pelosi kuzuru Syria!

1 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CCDd

Spika wa Baraza la Wawakilishi nchini Marekani bibi Nancy Pelosi anatarajiwa kufanya ziara nchini Syria licha ya upinzani mkali wa utawala wa rais Bush.

Bibi Pelosi ataongoza ujumbe wa wabunge wa Marekani utakaokutana na wajumbe wa serikali ya Syria.

Bibi Pelosi ni kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu katika bunge la Marekani kufanya ziara nchini Syria tokea kuanza kuvurugika kwa uhusiano baina ya Marekani na Syria.

Marekani ilomwondoa balozi wake kutoka Syria miaka 2 iliyopita baada ya kuuawa aliyekuwa waziri mkuu wa Lebanon Rafik Hariri. Syria ilihusishwa na mauaji hayo,lakini nchi hiyo imekanusha madai hayo.