1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Mataifa 11 ya kiarabu kualikwa katika mkutano wa amani ya mashariki ya kati

24 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBNB

Marekani imesema kuwa itayaalika mataifa 11 ya nchi za kiarabu zikiwemo Syria na Saudi Arabia katika mkutano wa kutafuta amani mashariki ya kati baadaye mwaka huu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Condoleza Rice kwa sasa anaainisha agenda za mkutano huo atakazowapa wawakilishi wa nchi zilizo mstari mbele katika suluhisho la mzozo wa mashariki ya kati, wanaoudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Aidha wanadiplomasia kutoka kundi la pande nne pia wataalikwa katika mkutano huo utakaojadili suluhisho la mzozo wa Palestina na Israel.Kundi hilo linajumuisha Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Urusi na Marekani yenyewe..

Wakati huo huo Israel imesema kuwa itawaachia huru wafungwa 90 wa kipalestina kati ya maelfu inawaowashikilia.

Baraza la mawaziri limekubaliana kuwaachia wafungwa hao ikiwa ni njia ya kumuunga mkono Rais Mahamoud Abbas wa mamlaka ya Palestina anayeungwa mkono na nchi za magharibi.

Kuna zaidi ya wafungwa elfu 10 wa kipalestina wanaoshikiliwa katika magereza ya Israel.