WASHINGTON:Marekani yaitaka Sudan ikubali majeshi ya UN kufikia mwisho wa mwaka huu | Habari za Ulimwengu | DW | 21.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Marekani yaitaka Sudan ikubali majeshi ya UN kufikia mwisho wa mwaka huu

Afisa wa ngazi ya juu wa Marekani ameionya serikali ya Sudan kwamba lazima ikubali kupelekwa kikosi cha Umoja wa mataifa katika jimbo la mzozo la Darfur kufikia mwishoni mwa mwaka huu la sivyo ichukuliwe hatua na jumuiya ya kimataifa.

Mjumbe maalum wa Marekani juu ya Sudan Andrew Natsios amewafahamisha viongozi wa serikali ya Sudan kuwaruhusu baadhi ya wanajeshi na wafanyikazi wa kiraia walioko Khartoum kuingia Darfur.

Ameitolea mwito Sudan kukubali kwa maandishi mpango wa baraza la usalama la umoja wa mataifa la kupeleka kikosi cha wanajeshi 20 elfu katika jimbo hilo ili kuzuia machafuko.Wakati huohuo mashambulio dhidi ya wafanyikazi wa mashirika ya kutoa msaada kwenye jimbo hilo yamesababisha kuondoka kwa wafanyikazi 71 na kuzuia msaada kuingia kwenye eneo la mji wa Gereida.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com