1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Marekani na Iran kukutana juu ya Iraq

14 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC2K

Marekani na Iran zinapanga kuandaa mazungumzo ya kihistoria katika wiki chache zijazo kujadili juu ya hali ya usalama nchini Iraq.

Msemaji wa ikulu ya Marekani Gordon Johndroe amethibitisha tangazo hilo lilotolewa kwanza na wizara ya mambo ya nje ya Iran jana jumapili.

Kwa mujibu wa msemaji huyo wa Ikulu ya Marekani lengo la mkutano huo utakaofanyika mjini Baghdad ni kuangalia jinsi gani serikali ya mjini Tehran itakavyoweza kusaidia kuweka mambo sawa nchini Iraq.

Katika miezi ya karibuni Washington imekuwa ikiishutumu Iran kwa kuchochea machafuko nchini Iraq.

Mkutano huo kati ya Marekani na Iran utakuwa wa kihistoria kwani nchi hizo mbili hazijakuwa na uhusiano wa kidiplomasia kwa zaidi ya miaka 25.