1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Marekani kulifikiria ombi la Uingereza

8 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbG

Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani imesema itafikira ombi la Uingereza la kutaka wakaazi wake watano wanaozuiliwa katika jela ya Guantanamo Bay waachiwe huru.

Wachambuzi wanasema kwamba hatua hiyo inadhihirisha kuwa waziri mkuu wa Uingerza Gordon Brown ana msimamo huru kwa Marekani tafauti na mtangulizi wake Tony Blair.

Awali serikali ya Uingereza iliingilia kati kesi dhidi ya raia wake waliozuiliwa katika jela hiyo ya Guantanamo lakini ilikataa kujihusisha na kesi za wakaazi wake wa kigeni ambao sio raia wa Uingereza.