WASHINGTON:Marekani haijapata uthibitisho iwapo Korea ya kaskazini imeanza kufunga kinu cha nyuklia | Habari za Ulimwengu | DW | 18.04.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Marekani haijapata uthibitisho iwapo Korea ya kaskazini imeanza kufunga kinu cha nyuklia

Marekani imesema haijapata uthibitisho iwapo Korea ya kaskazini imeanza kuufunga mtambo wake wa nyuklia.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani ameeleza hayo kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba yumkini Korea imeshaanza kuufunga mtambo wake wa nyuklia wa Yongbyong.

Korea ya kaskazini ilipaswa kuanza kukifunga kinu chake cha nyuklia jumamosi kwa mujibu wa mapatano yaliyofikiwa baina yake na jumuiya ya kimataifa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com