WASHINGTON:Bush na Olmert wajadili mzozo wa Palestina na Israel | Habari za Ulimwengu | DW | 20.06.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON:Bush na Olmert wajadili mzozo wa Palestina na Israel

Rais Gorge W Bush wa Marekani na waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert kwa mara nyingine tena wamesema wanaunga mkono suluhisho la kuwepo mataifa mawili katika mzozo wa Israel na Palestina.

Rais Gorge Bush pia alizitaka nchi za kirabu kutia juhudi katika kuusghulikia mzozo huu.

Wakizungumza mjini Washington Olmert na Bush walitoa ahadi za kumuunga mkono rais Mahmoud Abbas wa mamlaka ya wapalestina ambaye hivi karibuni ameteua serikali ya dharura baada ya kuivunja serikali iliyokuwa ikiongozwa na kundi la Hamas.

Marekani na Umoja wa Ulaya wamerudisha misaada kwa wapalestina kuanzia jumatatu kuonyesha uungaji mkono wao kwa rais Mahmoud Abbas.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com