1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON:Bush asisitiza kuweka makombora Ulaya Mashariki

17 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBhl

Rais George Bush wa Marekani na Lech Kaczynski wa Poland wameahidi kuendelea na mpango wa Marekani wa kuweka makombora ya kujihami Ulaya ya Mashariki pamoja na upinzani kutoka Urusi.

Akizungumza katika mkutano wao wa pamoja, Rais Bush amesema kuwa mpango huo wa kuweka makombora ya kujihami ni ishara ya amani na usalama.

Marekani inataka kuweka makombora kumi ya kujihami nchini Poland na mtambo wa rada huko Jamuhuri ya Czech katika kile inachosema kujihami na mashambulizi ya makombora ya Korea Kaskazini na Iran.

Hapo siku ya Jumamosi, Urusi ilisitisha ushiriki wake katika mkataba wa kudhibiti silaha na majeshi wa ulaya, ikiwa ni hatua ya upinzani dhidi ya mpango huo wa Marekani.