1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Wolfowitz ataondoka madarakani Juni 30

18 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC10

Rais wa Benki ya Dunia,Paul Wolfowitz atangatuka madarakani mwisho wa mwezi Juni.Tangazo hilo limetolewa siku chache baada ya jopo maalum kutoa ripoti iliyosema kwamba Wolfowitz alivunja maadili ya benki hiyo.Kiongozi huyo alikuwa akishinikizwa ajiuzulu kwa sababu ya kumpandisha cheo na kumpa nyongeza nono ya mshahara mpenzi wake,muda mfupi tu baada ya Wolfowitz kujiunga na Benki ya Dunia miaka miwili iliyopita.Msemaji wa Rais George W.Bush amearifu kuwa hivi karibuni Bush atamtaja yule atakaechukua nafasi ya Wolfowitz kama rais wa Benki ya Dunia.