WASHINGTON: Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marakeni, Condoleeza Rice, atarajiwa kuzuru Mashariki ya Kati. | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marakeni, Condoleeza Rice, atarajiwa kuzuru Mashariki ya Kati.

default

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Bi Condoleeza Rice, amenukuliwa akisema kwamba agizo la hivi karibuni la kukabiliana na wanamgambo wa Iran nchini Iraq, lilitolewa na Rais George W. Bush.

Bi Condoleeza Rice ameliarifu gazeti la New York Times kwamba uamuzi wa kukabiliana na mitandao ya Iran unajumuishwa na harakati za kijeshi zinazoendelea nchini Iraq.

Serikali ya Marekani inaishutumu Iran kwa kuwafadhili kifedha na pia kuwapa silaha wanamgambo wa kishia.

Bi Rice anatarajiwa kuzuru mashariki ya kati kwa juma moja kwa nia ya kufufua mashauriano ya amani kati ya Israil na Wapalestina.

Bi Condoleeza Rice atazitembelea Misri, Jordan, Saudi Arabia na Kuwait.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com