1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Waziri abakia kimya kuhusu Somalia

3 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBvL

Waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates,amekataa kusema cho chote kuhusu ripoti ya mashambulizi yaliolenga vituo nchini Somalia. Hapo awali,stesheni ya televisheni CNN iliripoti kuwa manowari ya jeshi la wanamaji la Marekani ilirusha makombora dhidi ya vituo vilivyoshukiwa kuwa vya Al-Qaeda,kaskazini mwa Somalia.Wakazi wamesema,waliona makombora yakishambulia maeneo ya milimani yaliyokaliwa na wanamgambo wa kigeni. Kwa hivi sasa,hakuna ripoti kuhusu hasara iliyosababishwa na mashambulizi hayo.