WASHINGTON: Wabunge wa Marekani waikataa ripoti ya jenerali Petreaus | Habari za Ulimwengu | DW | 12.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Wabunge wa Marekani waikataa ripoti ya jenerali Petreaus

Wabunge wenye ushawishi mkubwa wa vyama vya Democtratic na Republican nchini Marekani wameikataa ripoti iliyotolewa na kamanda mkuu wa jeshi la Marekani nchini Irak, David Petreaus inayotathimini hali nchini Irak.

Jenerali Petreaus na balozi wa Marekani nchini Irak, Ryan Crocker, wamekabiliwa na malalamiko ya wabunge kwamba hatua ya kuongeza idadi ya wanajeshi nchini Irak imeshindwa kutimiza lengo lake kubwa la kuleta upatanisho wa kisiasa.

Mgombea wa urais wa chama cha Democratic, Barack Obama, amesema ni makosa kuiwasilisha ripoti kuhusu hali nchini Irak katika siku iliyojaa huzuni ya shambulio baya zaidi la kigaidi kuwahi kufanywa duniani akisema kufanya hivyo ni kujaribu kudhihirisha kwamba uamuzi wa kwenda vitani nchini Irak unahusiana na mashambulio ya Septemba 11 mwaka wa 2001 nchini Marekani.

Aidha Barack Obama amesema

´Tumeweka sasa kipimo kuw achini mno kiasi cha kuuita ufansi katika hali iliyo mbaya kabisa. Imefikia kiwango ambapo sasa machafuko mengi yasoweza kuvumilika yaliyokuwepo mwezi Juni mwaka jnana wa 2006 yanaelezwa kuwa ufanisi. Na si hivyo.

Hili linaendelea kuwa kosa kubwa la sera ya kigeni.´

Mbunge wa chama cha Democratic, Joseph Biden amesema juhudi za Marekani nchini Irak zimeshindwa hivyo kutofautiana na matamshi ya jenerali Petreaus aliyesisitiza ufanisi umepatikana nchini Irak.

Chama cha Democratic kimesema mkakati mpya wa jenerali Petraeus unaashiria miaka mingine kumi ya vita nchini Irak huku rais George W Bush akitarajiwa kulihutubia taifa hii leo katika ikulu yake mjini Washington.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com