1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Vikao vya siri kwa watuhumiwa wa ugaidi

10 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCKZ

Marekani imeanza vikao vya siri vya kijeshi huko Guantanamo kuyakinisha iwapo watuhumiwa wakuu 14 wa ugaidi wanaowana na sifa yake ya kisheria kuitwa kuwa wapiganaji maadui.

Watuhumiwa hao ni pamoja na Khalid Sheikh Mohammed anayedaiwa kwa mpangaji wa mashambulizi ya kigaidi kwa kuteka nyara ndege ya Septemba mwaka 2001 mjini New York.Mtuhumiwa mwengine ni Hambali kiongozi wa kundi la kusini mashariki mwa Asia anayelaumiwa kuhusika na uripuaji wa mabomu wa Bali nchini Indonesia mwaka 2002.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani imekuwa ikiwapiga marufuku waandishi wa habari huko Guantanamo kambi ya kijeshi ya Marekani ilioko nchini Cuba.

Watuhumiwa hao wamekuwa hawana mawasiliano na mawakili badala yake wamekuwa wakipatiwa washauri wa kijeshi. Wizara ya ulinzi ya Marekani imesema kile kinachoendelea mbele ya jopo hilo la maafisa watatu wa kijeshi kitahaririwa kabla ya kutolewa hadharani.

Wataalamu wa haki za binaadamu wameshutumu utaratibu huo.