1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Tetemko la ardhi kisiwani Hawai

16 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD2O

Kumetokea tetemeko la ardhi katika kisiwa cha Hawai nchini Marekani. Tetemeko hilo ambalo limefikia kiwango cha 6.6 kwenye kipimo cha Richter, limearifiwa na Marekani kuwa kubwa na kwamba limesababisha umeme kukatika na kuwajeruhi watu kadhaa ambao wanatibiwa katika hospitali. Taarifa hizo za mwanzo hazikutaja maafa yoyote lakini wataalamu wa hali ya hewa wameonya juu ya uwezekano wa kutokea tetemeko baya zaidi hii leo, ila sio Tsunami.