1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Rice aionya Iran baada ya jaribio la kombora

3 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwZ

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice ameikaripia Iran kwa kujaribu kuonyesha ubabe baada ya kufyetuwa kombora jipya la masafa marefu kwa mara ya kwanza hapo jana na kuionya serikali ya nchi hiyo kwamba itateseka vibaya sana iwapo itatumia silaha kwa hasira.

Vikosi vya Iran vimefyatuwa kombora la Shahab nambari 3 wakati vilipokuwa vikianza mazoezi ya kivita ya siku 10 ambayo yanakwenda sambamba na harakati zinazoongozwa Marekani kuweka vikwazo vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran kutokana na mpango wake wa nuklea.

Akizungumza katika mahojiano ya radio Rice amesema anafikiri pia kwamba Wairan hawatambui hali ya usalama ni ile ambayo iwapo watajaribu kufanya jambo fulani nchi hiyo ndio itakayoathirika vibaya.

Rice amelitafsiri jaribio hilo la kombora kuwa ni ujumbe wa Iran kwa dunia kwamba haiwezi kuwazuwiya kuwa na silaha za nuklea.