Washington: Rais George W. Bush kutaka mkakati wake mpya kuhusu Iraq juma lijalo. | Habari za Ulimwengu | DW | 05.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Washington: Rais George W. Bush kutaka mkakati wake mpya kuhusu Iraq juma lijalo.

Rais George W. Bush amesema adhabu dhidi ya Saddam Hussein ilipaswa kutekelezwa kwa nidhamu nzuri.

Hata hivyo, Rais Bush amesema rais huyo wa zamani wa Iraq alitendewa haki ambayo hakuwatendea mamia ya raia wake.

Rais George Bush aliahidi atatoa taarifa juma lijalo kuhusu mkakati wake mpya nchini Iraq.

Rais George Bush alisema:

"Ninazingatia hilo sana. Juma lijalo nitakuwa tayari kueleza mkakati utakaowasaidia raia wa Iraq kupata serikali watakayoweza kusimamia. Ningali nikashauriana na wahusika"

Wakati huo huo, walinzi wawili wamekamatwa kwa tuhuma za kupiga picha za ukanda wa video zilizoonyesha yaliyotokea wakati wa kunyongwa Saddam Hussein.

Maafisa wa Iraq wameahirisha tarehe ya kunyongwa wasaidizi wa Saddam Hussein hadi siku ya Jumapili ijayo.

Ndugu wa kambo wa Saddam na Jaji wa zamani wa mahakama ya Iraq walipaswa kutiwa kitanzi jana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com