WASHINGTON : Rais Castro yuko mahtuti | Habari za Ulimwengu | DW | 15.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON : Rais Castro yuko mahtuti

Mkuu wa shughuli za ujasusi chini Marekani amesema katika mahojiano yaliochapishwa leo hii kwamba Rais Fidel Castro wa Cuba yuko mahtuti na anakaribia kufa.

John Negroponte ameliambia gazeti la Washington Post kwamba kila kitu wanachokiona kinaashiria hautopita muda mrefu na kwamba ni suala la miezi tu na sio miaka kiongozi huyo wa Cuba atautema.

Castro mwenye umri wa miaka 80 hakuonekana hadharani tokea afanyiwe operesheni ya utumbo na kukasimu kwa muda madaraka yake ya urais kwa kaka yake mdogo Raul Castro hapo tarehe 31 mwezi wa Julai.

Castro amekuwepo madrakani kwa miaka 35.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com