1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Nchi za Ulaya zimelengwa kushambuliwa na Al-Qaeda

Mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda una mpango wa kushambulia usafari wa ndege na reli barani Ulaya.Stesheni ya televisheni ya Marekani CBS imesema,mashirika ya upelelezi yamepata habari hiyo baada ya kuwahoji washukiwa wa ugaidi waliotoka Afghanistan na Pakistan hivi karibuni. Kwa mujibu wa washukiwa hao,mtandao wa al-Qaeda unataka kufanya mashambulio ya bomu kwenye ndege zinazovuka bahari ya Atlantik sawa na yale mashambulio yaliozuiliwa mwezi wa Agosti nchini Uingereza.Ripoti hiyo inalingana na ripoti za upelelezi kuwa Al-Qaeda,inawaondosha wapiganaji wake wa kigeni wenye asili ya Kiarabu pamoja na wataalamu wa mikakati,kutoka sehemu za milimani huko Afghanistan.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com