WASHINGTON: Mwanafunzi wa nne mhanga wa shambulio la shule nchini Marekani afariki dunia | Habari za Ulimwengu | DW | 03.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Mwanafunzi wa nne mhanga wa shambulio la shule nchini Marekani afariki dunia

Idadi ya wanafunzi waliyokufa katika mauwaji yaliyotokea katika shule mmoja katika jimbo la Pennsylvania nchini Marekani imeongezeka na kufikia watu wanne baada ya mwanafunzi wa kike aliyekuwa amelazwa katika hospitali kufariki dunia. Mtu aliyekuwa na bunduki hivi karibuni aliwateka nyara wanafunzi kutoka jamii ndogo ya Amish katika kijiji cha Paradise na kuwauwa wasichana watatu baada ya kuwaachilia huru wavulana wote na kwisha kujiuawa kwa risase.

Shambulio hilo ni na tatu lililolenga shule na kusababisha mauwaji kwa muda wa wiki mmoja tu.

Pia limetokea baada ya onyo 4 za tahadhari katika shule mbili katika jimbo jingine la Nevada.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com