1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Mnara wa kumkumbu wa Mchungaji King

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsu

Takriban wanasiasa 5,000,watu mashuhuri na raia wa kawaida wamekusanyika katika mji mkuu wa Marekani Washington ambapo ujenzi unaendelea wa mnara wa kumbukumbu kumuenzi Mchungaji Martin Luther King Jr.

Mnara huo wa kumbukumbu wa Mchungaji King utasimama kati ya kumbukumbu za marais Jefferson na Lioncoln na utakuwa mnara wa kwanza kabisa wa kumbukumbu kuwepo katika eneo la kumbukumbu la taifa kumuenzi Mmarekani mweusi.

Wazungumzaji katika hafla hiyo walikuwa ni pamoja na Rais George W Bush na Rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ambao walipongeza imani ya Luther King Jr kwamba maandamano yasio na matumizi ya nguvu yanaweza kusaidia kukomesha ubaguzi wa rangi.

Ujenzi wa mnara huo unatarajiwa kukamilika hapo mwaka 2008 miaka 40 baada ya King kuuwawa huko Memphis katika jimbo la Tennessee.