1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Mauaji ya kampuni ya Black Water yachunguzwa

20 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CPar

Mahakama ya Marekani inachunguza jukumu la kampuni ya usalama ya Black Water Worldwide katika mauaji ya Wairaki 17 waliopigwa risasi na maafisa wa kampuni hiyo mjini Baghdad.

Walinzi wa kampuni ya Black Water waliohusika katika kisa hicho kilichotokea mnamo tarehe 16 mwezi Septemba mwaka huu katika uwanja wa Nisoor magharibi mwa mji mkuu Baghdad, hapo awali walipewa ulinzi dhidi ya kufunguliwa mashtaka na wachunguzi wa wizara ya mambo ya ndani ya Marekani kwa ushuhuda walioutoa kuhusina na mauaji ya Wairaki hao.