1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yashinikiza vikwazo vipya dhidi ya Iran

16 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CImV

Marekani imesema,itashinikiza kuiwekea Iran vikwazo vipya,kufuatia ripoti iliyotolewa na Shirika la Nishati ya Nyuklia la Umoja wa Mataifa-IAEA kuhusika na mradi wa nyuklia wa Iran.Shirika hilo la kimataifa katika ripoti yake kuhusu mpango wa kinyuklia wa Iran limesema, Tehran imetekeleza baadhi ya masharti,lakini inaendelea kupuuza mwito wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kusitisha harakati za kurutubisha madini ya uranium.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani,Dana Perino amesema,Washington katika mkutano wa juma lijalo pamoja na nchi nne zingine wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama na pamaoja na Ujerumani zitapanga vikwazo vipya vya dhidi ya Iran.