1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington. Marekani yakataa kuweka ulazima wa kila nchi kuweka viwango vya kupunguza gesi zinazochafua mazingira.

29 Septemba 2007
https://p.dw.com/p/CBLo

Rais wa Marekani George W. Bush amerudia msimamo wake wa kukataa kulazimika kwa kila nchi kuweka viwango vya kupunguza gesi zinazoharibu mazingira wakati akihutubia mkutano wa mataifa 16 yanayotoa gesi hizo kwa wingi mjini Washington.

Bush amesema kuwa nchi yake inalichukulia suala la ongezeko la ujoto duniani kwa dhati, lakini hatua za kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa hazistahili kuzuwia ukuaji wa uchumi.

Hatua hii mpya inapaswa kujumuisha watoaji wote wakubwa duniani wa gesi zinazoharibu mazingira ikiwa ni pamoja na mataifa yaliyoendelea na yale yanayoendelea. Tutaweka lengo la muda mrefu la utoaji wa gesi zinazoharibu mazingira duniani. Kila nchi itaweka mkakati wake binafsi wa kitaifa katika kupiga hatua za maendeleo kuelekea kupata mafanikio katika lengo hili la muda mrefu.

Pi ameweka msisitizo mkubwa katika nishati ya kinuklia kuwa ni chanzo cha nishati safi. Wakosoaji wa mkutano huo ulioitishwa na Bush wanasema kuwa unakinza juhudi za umoja wa mataifa za kuweka malengo maalum yatakayotekelezwa kwa pamoja ya kupunguza utoaji wa gesi hizo kuwa badala ya mkataba wa Kyoto wakati utakapomalizika muda wake mwaka 2012.