WASHINGTON: Marekani yaionya Ulaya kutotoa maoni juu ya hukumu ya kifo ya Saddam Hussein | Habari za Ulimwengu | DW | 07.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Marekani yaionya Ulaya kutotoa maoni juu ya hukumu ya kifo ya Saddam Hussein

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani bibi, Condoleeza Rice, amezitolea mwito nchi za Ulaya kutotoa maoni yoyote juu ya hukumu ya kifo iliotolewa dhidi ya rais wa zamani wa Irak, Saddam Hussein. Bibi Rice alisema hatua inawahusu wairaki wenyewe. Halmashauri ya Ulaya na nchi kadhaa wanachama wa Umoja wa Ulaya, ziliikosoa hukumu hiyo kwamba adhabu ya kifo ni jambo lisilokubalika.

Mahakama kuu nchini Irak ambayo inagahrimiwa na kushauriwa na Marekani, ilimkuta Saddam Hussein na hatia ya uvunjaji haki za binaadamu kwa mauaji ya raia wa kishiha 148 katika kijiji cha Dujail mnamo mwaka 1982. Kesi ya pili inaomkabili Saddam Hussein, inatarajiwa kuendelea kusikilizwa leo. Kesi hiyo inahusu maovu yaliotendewa wakurdi yakizingatiwa mauaji ya raia katika kijiji cha Anfal.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com