1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani yafikiria kurekebisha mkakati wa Irak

11 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCts

Baada ya kujiuzulu kwa waziri wa ulinzi wa Marekani Donald Rumsfeld,viongozi wa majeshi ya Marekani wanachunguza mkakati wao nchini Irak. Jemadari mkuu Peter Pace,amedokezea juu ya kurekebishwa kwa utaratibu,lakini hakutoa maelezo zaidi.Amesema,ikiwa kumefanywa makosa,ni lazima kutambua ukweli huo na marekebisho yanayohitajiwa yafanywe ili kutekeleza malengo yaliopangwa. Wakati huo huo,wizara ya ulinzi-Pentagon mjini Washington imesema,wanajeshi wenye uzoefu huko Irak watashauriwa vile vile.