1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Marekani kupeleka wanajeshi wengine 35,000 Iraq

9 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC3s

Wizara ya ulinzi nchini Marekani-Pentagon imetangaza kuwa vikosi vingine 10 vimepokea amri ya kwenda Irak.Msemaji wa wizara hiyo,Bryan Whitman amesema,vikosi hivyo vya kama wanajeshi 35,000 vitapelekwa Irak mwaka huu,kati ya mwezi wa Agosti na Desemba.Akaeleza kuwa vikosi hivyo vitaisaidia Marekani kuimarisha kiwango cha majeshi yake nchini Irak,angalao hadi mwishoni mwa mwaka 2007.