1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Malkia Elizabeth yuko Marekani

4 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC51

Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza amewasili nchini Marekani kwa ziara rasmi ya siku sita.

Malkia yuko katika jimbo la Virginia kuadhimisha miaka 400 ya makaazi ya kwanza ya walowezi wa Uingereza ya mji wa Jamestown.Maelfu walimlaki Malkia nje ya jengo la bunge la jimbo la Virginia.Ameanza ziara yake hiyo ya nne kwa ujumla nchini Marekani kwa kuhutubia bunge la jimbo hilo.

Mwanzoni mwa hotuba yake ametowa heshima zake kwa walioathirika na mauaji ya Chuo Kikuu cha Virginia mwezi uliopita.