1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Majeruhi jeshini wamepewa tiba ya hali ya chini

3 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMw

Katibu wa majeshi ya Marekani,amejiuzulu kuhusika na lawama kuwa wanajeshi wa Kimarekani waliojeruhiwa hupewa matibabu ya hali ya chini.Kujiuzulu kwa Francis Harvey kulitangazwa na waziri wa ulinzi wa Marekani, Robert Gates siku moja baada ya mkuu wa kituo cha kijeshi cha matibabu kufukuzwa kazi.Juma lililopita,gazeti la “Washington Post“ liliripoti kuwepo kwa hali za chini za tiba katika kituo cha “Walter Reed Army Medical Centre“ mjini Washington na kusema kwamba wanajeshi waliojeruhiwa Irak na Afghanistan,wamepewa matibabu katika majengo ambako panya na mende wametapakaa.Rais George W.Bush ameahidi kuwa suala hilo litachunguzwa na tume iliyo huru.