WASHINGTON: Kamanda wa jeshi la Marekani nchini Irak awasilisha ripoti yake bungeni | Habari za Ulimwengu | DW | 11.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Kamanda wa jeshi la Marekani nchini Irak awasilisha ripoti yake bungeni

Kamanda mkuu wa jeshi la Marekani nchini Irak, jenerali David Patraeus, amependekeza wanajeshi wa Marekani walio nchini Irak wapunguzwe kufikia msimu ujao wa kiangazi.

Wanajeshi 30,000 wa Marekani huenda wakaondolewa kutoka Irak kufikia katikati ya mwaka ujao 2008 na wanajeshi 2,000 huenda wakaanza kuondoka katika majuma machache yajayo.

Akiwasilisha ripoti yake katika bunge la Marekani, jenerali Petraeus, amesema malengo ya kijeshi kwa kiwango kikubwa yanafanikiwa na kwamba wanajeshi wa Marekani na wa Irak wamepata ufanisi mkubwa katika kudumisha usalama licha ya kukabiliwa na maadui hatari na joto kali la msimu wa kiaganzi nchini Irak.

Hata hivyo jenerali Petraeus ameonya kwamba hali bado ni ngumu nchini Irak na muda unahitajika kujatimiza malengo yanayonuiwa.

´Tukizingatia hali nchini Irak bado ni ngumu na mara nyingine ya kuvunja moyo. Pia ninaamini inawezekana kuyatimiza malengo yetu katika kipindi fulani ingawa kufanya hivyo hakutakuwa haraka wala rahisi.´

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com