1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Washington .Daraja laanguka na kuuwa watu.

2 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBd0

Nchini Marekani daraja moja limevunjika katika mji wa Minneapolis linalovuka katika mto Mississippi. Daraja hilo ambalo linabarabara nne zinazopita magari lilivunjika wakati wa majira ya jioni ambapo watu wanarejea kutoka kazini, na kusababisha magari kadha kutumbukia majini.

Picha za televisheni zinaonyesha madereva wakiwa wamekwama katika vipande vikubwa vya daraja hilo vilivyovunjika vikizungukwa na maji.

Magari kadha yalitupwa mtoni, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari nchini humo, na taarifa zinasema kuwa hadi sasa watu watatu wamefariki na wengine kadha wamejeruhiwa.

Sehemu za daraja hilo zimekuwa katika matengenezo. Ripoti za mwanzo zinasema kuwa njia moja tu ya daraja hilo iliruhusiwa kupita magari kila upande. Lakini magari yalikuwa yamesimama wakati wa ajali hiyo.