1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Daktari wa upasuaji katika hospitali ya kijeshi ajiuzulu

13 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCJd

Daktari mkuu wa upasuaji wa jeshi la Marekani amejiuzulu kufuatia kashfa katika hospitali ya kijeshi ya Marekani ya Walter Reed. Luteni jenerali Kevin Kiley ni kiongozi wa tatu wa cheo cha juu kupoteza kazi yake kufuatia habari kwamba wanajeshi wanaojeruhiwa nchini Irak na Afghanistan hawapati matibau mazuri katika hospitali hiyo.

Ripoti za hivi karibuni zilizotolewa na magazeti ya Marekani zilieleza hali mbaya katika hospitali hiyo, ikiwa ni pamoja na vyumba vilivyojaa panya na mende.