1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush hataki majadiliano ya moja kwa moja

14 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCsx

Rais George W.Bush wa Marekani ameikataa miito ya kuwa na mazungumzo mapya pamoja na Iran na Syria katika juhudi ya kutafuta amani katika Mashariki ya Kati.Kiongozi huyo wa Marekani vile vile amewatahadharisha Wademokrat dhidi ya kuchukua hatua ya haraka kupunguza vikosi vya Marekani nchini Irak.Bush alitamka hayo baada ya kuwa na mkutano wa faragha pamoja na kundi linalochunguza suala la Irak.Kundi hilo likiongozwa na waziri wa mambo ya kigeni wa zamani wa Marekani,James Baker na aliekuwa mbunge wa chama cha Demokrat-Lee Hamilton,mwezi ujao linatazamiwa kutoa ushauri wake kuhusu Irak.