WASHINGTON: Bush akataa kuwaondoa wanajeshi kutoka Irak | Habari za Ulimwengu | DW | 20.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

WASHINGTON: Bush akataa kuwaondoa wanajeshi kutoka Irak

Katika kuadhimisha miaka minne tangu uvamizi wa Irak ulioongozwa na Marekani rais George W Bush amekataa miito ya kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Irak.

Rais Bush ametaka kuwepo uvumilivu katika vita vya Irak huku akiwahimiza Wamarekani waupe mda mpango mpya wa usalama mjini Baghdad ufaulu.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Maekani, Condoleezza Rice, amesema mataifa jirani na Irak na jumuiya ya kimataifa inatakiwa kuisadia serikali ya mjini Baghdad.

´Majirani wa Irak pamoja na jumuiya ya kimataifa wana jukumu lililo wazi la kufanya kuziunga mkono juhudi za serikali ya Irak kudumisha amani na kuendeleza maridhiano nchini humo.´

Rais Bush amewataka wabunge wa chama cha Democtratic katika bunge la Congress wasilipinge ombi la fedha zinazohitajika katika vita nchini Irak.

Rais Bush ameutoa mwito huo sambasamba na ripoti ya maoni ya Wamarekani inayopendekeza kwamba Wairak wanaendelea kuwa na wasiwasi na wanaamini majeshi ya muungano yanasababisha kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama nchini Irak.

Waziri mkuu wa Uingereza bwana Tony Blair, mshirika mkubwa wa rais Bush katika vita vya Irak hakuwa na mawazo ya kuingia vitani wakati alipochaguliwa kuwa waziri mkuu mnamo mwaka wa 1997.

Kizazi changu ni cha kwanza kilichoweza kutafakari juu ya uwezekano wa kuishi bila kwenda vitani au kuwatuma watoto wetu vitani. Hiyo ni zawadi yenye thamani kubwa.´

Miaka minne ya vita vya Irak ikiadhimishwa hii leo, waziri mkuu Tony Blair amekabiliwa na upinzani mkali nchini Uingereza kwa kuviunga mkono vita vya Irak.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com