1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bush aidhinisha Dola bilioni 100 kugharimia vita

26 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CBy6

Rais George W.Bush wa Marekani ametia saini mswada unaoidhinisha kuongeza dola bilioni 100 kugharimia vita nchini Iraq na Afghanistan.Hatua hiyo imemaliza mgogoro wa miezi minne kati ya Bush na bunge linalodhibitiwa na chama cha Demokratik.Bunge lilitaka kupangwe tarehe ya kuvirejesha nyumbani vikosi vya Kimarekani kutoka Iraq.Pendekezo hilo limepingwa kabisa na Bush. Wakati huo huo maafisa wa Iraq na Uingereza wamesema,vikosi maalum wa vya Iraq vimempiga risasi na kumuua kamanda wa kundi la wanamgambo liitwalo “Jeshi la Mehdi” ambalo huongozwa na shehehe wa Kishia Moqtada al-Sadr.Saa chache baadae Moqtada al-Sadr alijitokeza hadharani kwenye msikiti wa mjini Kufa.Kiongozi huyo aliekuwa mafichoni tangu Oktoba mwaka jana, amekariri mwito wake wa kuwataka wanajeshi wa Kimarekani waondoke Iraq.