1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bunge la Marekani lapitisha mswada wa kuwaondoa wanajeshi kutoka Irak

30 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEB

Bunge la Marekani limepitisha mswada ambao huenda ukaitaka serikali iwaondoe wanajeshi wa Marekani walio nchini Irak kufikia mwezi Machi mwaka wa 2008, kama sharti la kuidhinisha fedha zaidi katika vita nchini Irak na Afghanistan.

Wabunge 51 waliunga mkono mswada wa kuongeza bajeti ya gharama za vita hadi kufikia dola bilioni 122, licha ya rais George Bush kutishia kutumia kura yake ya turufu kuutilia guu mswada huo. Wabunge wengine 47 waliupinga mswada huo.

Hapo awali rais Bush alikutana na wabunge wa chama cha Republican katika baraza la wawakilishi kutafuta kuungwa mkono katika msimao wake juu ya mswada huo. Wiki iliyopita, baraza hilo lilipitisha mswada unaoweka mwezi Septemba mwaka ujao kama tarehe ya mwisho ya kuondoka wanajeshi wa Marekani walio nchini Irak.