1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON : Bunge la Marekani lamkaidi Bush

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6h

Katika dharao isio na kifani kwa sera ya vita ya Rais George W. Bush bunge la Marekani hapo jana limeidinisha muswada wa sheria ambao unahusisha kuondolewa kwa wanajeshi wa Marekani nchini Iraq na kugharamia vita.

Kwa kura 51 dhidi ya 46 baraza la Senate limeungana na baraza la wawakilishi la bunge la Marekani katika kuunga mkono muswada huo ambao utatowa dola bilioni 100 kwa ajili ya vita nchini Iraq na Afghanistan mwaka huu wakati ukiweka tarehe ya mwisho ya kuwaondowa wanajeshi wa Marekani kutoka Iraq katika kipindi cha miezi 11 ijayo.

Hiyo ni mara ya kwanza kwamba bunge lote ambalo limekuwa likidhibitiwa na chama cha Demokrat tokea mwezi wa Januari kumkaidi rais.

Bush amekuwa akisema mara kwa mara kwamba katu hatokubali kuwekewa tarehe ya kusalimu amri na Ikulu ya Marekani imesema ataupigia kura ya turufu muswada huo.