1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WASHINGTON: Bibi Hillary Clinton aanza harakati kuelekea uchaguzi wa urais wa Marekani

21 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCZC

Seneta wa chama cha Demokratic, Hillary Clinton, amepiga hatua ya kwanza katika harakati zake za kujaribu kuwa rais wa kwanza mwanamke kuchaguliwa nchini Marekani.

Kwenye ujumbe wa sauti ulioko katika ukurasa wake kwenye mtandao, Bi Hillary Clinton, mwenye umrí wa miaka hamsini na tisa, ametoa wito kwa wapiga kura kuanza majadiliano pamoja naye kuhusu maswala yanayolikumba taifa la Marekani.