1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wasemavyo wahariri

Oumilkher Hamidou21 Septemba 2010

Mkutano wa kilele wa malengo ya maendeleo ya millenia na shauri la SPD la kutaka wananchi waulizwe maoni kama vinu vya nishati ya kinuklea viendelee kutumika ni miongoni mwa mada magazetini

https://p.dw.com/p/PI62
Makao makuu ya Umoja wa mataifa mjini New YorkPicha: picture alliance/dpa

Tuanzie lakini New York unakoendelea mkutano wa kilele unaotathmini uwezekano wa kufikiwa malengo ya maendeleo ya Millenia hadi ifikapo mwaka 2015.Gazeti la "Flensburger Tageblatt" linaandika:

"Thuluthi mbili ya muda uliowekwa imeshamalizika,ishara ya kufikiwa malengo yaliyowekwa lakini haijachomoza.Kinyume kabisa.Yadhihirika kana kwamba wahusika wamepotea njia.Jumuia ya kimataifa ilidhamiria kupunguza kwa nusu hadi ifikapo mwaka 2015, idadi ya watu maskini duniani,kupunguza kwa thuluthi mbili idadi ya vifo vya watoto na kupiga hatua muhimu katika kupambana na ukimwi,Malaria kifua kikuu na maradhi mengineyo.Hii leo yadhihirika kana kwamba malengo hayo hayawezi tena kufikiwa.Hata serikali kuu ya mungano wa nyeusi na manjano mjini Berlin haijatekeleza ipasavyo lengo la siasa yake ya maendeleo.Imeshindwa kutekeleza ahadi iliyotoa ya kutenga asili mia sifuri nukta 51 ya pato la ndani la taifa kugharimia misaada ya maendeleo.Hadi sasa wamefanikiwa kutoa asili mia sifuri nukta nne tuu .

Amoklauf Lörrach
Polisi wanalinda mlango wa kuingia katika hospitali ya St Elibateh huko Lörrach,kusini magharibi ya UjerumaniPicha: dapd

Baada ya kisa cha bibi mmoja, ambae ni wakili na mwanaspoti ,kijana wa miaka 41,kuwauwa kwanza mwanawe na mumewe wa zamani, na baadae kumwaga damu zaidi katika kijiji kidogo cha Lörrach,kusini magharibi ya Ujerumani,wahariri wanaendelea kujiuliza........Gazeti la "Stuttgarter Nachrichten" linaandika:

Jamii ya Ujerumani imeduwaa kutokana na maangamizi na uharibifu ulioanzia kwanza nyumbani dhidi ya mumewe mwenye umri wa miaka 44 na baadae mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka 5.Pengine bibi huyo amewauwa kwanza wote hao wawili kabla ya kuanza kuwashambulia wapita njia na kuingia katika hospitali ya St.Elisabeth na kumuuwa muuguzi mmoja.Tukio ambalo ,sawa na Winnenden na Wendlingen hakuna pia atakaelisahau milele huko Lörrach.

Mada yetu ya mwisho magazetini inahusu pendekezo la mwenyekiti wa chama cha upinzani cha Social Democratic,Sigmar Gabriel kutaka wananchi waulizwe maoni yao kama wanapendelea au la muda wa vinu vya nishati ya nuklea urefushwe.Gazeti la "Emder Zeitung "linaandika:

Si jambo jipya kuona vyama vinapokua upande wa upinzani,mara vinajiliwa na kiu cha kutaka wananchi waulizwe maoni yao.Hali hiyo inatokea zaidi wanapojua kwamba wananchi walio wengi watawaunga mkono.Kwakua hadi wakati huu,chama chochote kilichoko madarakani kimekua kikijizuia kulizusha suala la wananchi kuulizwa maoni yao.Kwa hivyo hata shauri hili la SPD halitaitikwa-na bora hivyo.Kuulizwa wananchi maoni yao ni suala la kimsingi na halistahiki kushughulikiwa kijuu juu.Na katika hali ya sasa ndiyo kabisa.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mpitiaji:Abdul-Rahman