1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

WARSAW:Katiba ya Umoja wa Ulaya bado ina utata

1 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCWE

Nchi ya Ujerumani inatangaza haitakamilisha mpango wake wa kuhakikisha kuwa rasimu katiba ya Umoja wa Ulaya inapatikana kabla muhula wake kama kiongozi wa Umoja huo unamalizika.Ujerumani ndiye kiongozi wa Umoja wa Ulaya kwa kipindi cha miezi sita.Kwa mujibu wa Waziri wa mashauri ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier kuna uwezekano mdogo sana wa hilo kufikiwa kwani rasimu ya katiba hiyo ilikataliwa na mataifa ya Ufaransa na Uholanzi katika kura ya maoni jambo linalozua mkwamo wa kisiasa.

Ujerumani imekuwa ikifanya majadiliano kuhusu katiba hiyo na kutaraji itaweza kuzindua mpango utakaoweza kufanikisha shughuli hiyo ili kuepuka mkwamo katika maamuzi ya muungano huo.Muungano wa Ulaya kwa sasa unapanuka na kuongeza nchi mpya wanachama hasa kutoka Ulaya mashariki.

Nchi ya Poland iliyojiunga na Umoja huo mwaka 2004 bado haijaidhinisha pendekezo la katiba hiyo.Mataifa mengine tisa kutoka Ulaya Mashariki yalijiunga na Umoja huo wakati huo.Nchi ya Ujerumani kama mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya inalenga kuimarisha uhusiano kati ya wanachama na mataifa jirani yaliyokuwa ya kikomunisti ya Ukraine na Georgia.