Warsaw.Jaroslaw kuizuru Ujerumani leo. | Habari za Ulimwengu | DW | 30.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Warsaw.Jaroslaw kuizuru Ujerumani leo.

Waziri mkuu wa Poland Jaroslaw Kaczynski, anaanza ziara ya kwanza rasmi nchini Ujerumani hii leo.

Mada kuu wakati wa mazungumzo kati ya kiongozi huyo wa Poland na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ni nishati.

Poland imekataa mradi wa pamoja kati ya Ujerumani na Urusi wa kujenga bomba la gesi litakalopita chini ya bahari ya Baltic na siyo katika ardhi ya nchi hiyo.

Kabla ya ziara yake hii, waziri mkuu Kaczynski alikana taarifa kwamba uhusiano kati ya Ujerumani na Poland umeharibika.

Kansela Merkel anatumaini kuwa ziara hii itaimarisha uhusiano kati ya nchi hizo jirani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com