1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapiga kura wachagua bunge jipya Afghanistan

18 Septemba 2010

Uchaguzi wa bunge la Afghanistan umemalizika. Licha ya mashambulizi ya Wataliban, wapiga kura walijitokeza kuchagua bunge jipya. Watu wanane wameuawa katika mashambulizi hayo.

https://p.dw.com/p/PFj9
Afghan women wait outside a polling booth during the parliamentary elections in Kabul, Afghanistan, Saturday, Sept. 18, 2010. (AP Photo/Saurabh Das)
Wanawake wa Afghanistan wakingojea kupiga kura katika uchaguzi wa bunge mjini Kabul, Septemba 18, 2010.Picha: AP

Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Ndani katika mji mkuu Kabul imesema kuwa imeridhika na zoezi hilo la uchaguzi.

Afghan President Hamid Karzai speaks at a meeting with tribal leaders in Kandahar city, Afghanistan, Sunday June 13, 2010. President Karzai appealed to hundreds of tribal and religious leaders to support a major operation in their southern province, the heartland of a Taliban insurgency. Karzai, accompanied by top NATO commander US General Stanley McChrystal, spoke to representatives and residents in Kandahar about renewed efforts to bring stability to the war-weary province. (AP Photo//Massoud Hossaini, Pool)
Rais wa Afghanistan,Hamid Karzai.Picha: AP

Muda mfupi tu baada ya kufunguliwa kwa vituo vya kupigia kura, Rais Hamid Karzai mara nyingine tena alitoa mwito kwa Waafghanistan kujitokeza kupiga kura zao.

Wagombea 2,500 wamewania viti 248 bungeni katika uchaguzi mkuu wa pili kufanywa nchini humo tangu serikali ya Taliban kupinduliwa mwaka 2001. Uchaguzi huo umefanywa chini ya ulinzi mkali.

Kiasi ya watu milioni 10.5 wamekuwa na haki ya kupiga kura katika uchaguzi huo unaotazamwa kama ni mtihani mkuu wa utulivu na mchakato wa kidemokrasia nchini Afghanistan.Matokeo ya uchaguzi hayatazamiwi kabla ya mwisho wa mwezi wa Oktoba.

Mwandishi: P.Martin/ ZPR

Mpitiaji: M.Dahman