1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Waperu walalamika misaada inakawia

P.Martin18 Agosti 2007

Siku mbili baada ya kutokea tetemeko la ardhi nchini Peru,mitetemeko mingine iliyofuatilia, imeitikisa nchi hiyo siku ya Ijumaa.Hasara iliyosababishwa na mitetemeko iliyofuatia haijulikani.

https://p.dw.com/p/CB1w
Familia ikikaa kando ya nyumba yao iliyoteketezwa na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea siku ya Jumatano
Familia ikikaa kando ya nyumba yao iliyoteketezwa na tetemeko kubwa la ardhi lililotokea siku ya JumatanoPicha: AP

Tetemeko kubwa la siku ya Jumatano,limeua hadi watu 510 na kama 1,500 wengine wamejeruhiwa.Vile vile maelfu ya watu wamepoteza makazi yao.Maafisa nchini Peru wana hofu kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka kwa sababu ni shida kwenda katika vijiji vingi vilivyotengwa kutokana na uharibifu wa tetemeko la ardhi la siku ya Jumatano.

Walionusurika wanalalamika kuwa misaada ya dharura inakawia kuwafikia na baadhi yao wamepora maduka ya dawa na kupigana katika foleni za kungojea chakula.Kamisheni ya Umoja wa Ulaya inatoa msaada wa dharura wa Euro milioni moja.