1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapatanishi wa migogoro wakutana wabadilishane mawazo huko Zanzibar

24 Aprili 2007

Taasisi ya Mashauriano ya maswala ya kibinadamu yenye makao yake mjini Geneva na wakfu wa Mwalimu Nyerere nchini Tanzania zimeandaa mkutano wa siku tatu katika visiwa vya Zanzibar.

https://p.dw.com/p/CHFZ

Mkutano huo unawajumuisha wapatanishi watakaoijadili changamoto zinazosababishwa na vita barani Afrika na wakati huo huo kutafuta mbinu za kusuluhisha baina ya makundi yanayozozana duniani kote.

Dr. Salim Ahmed Salim mjumbe maalum wa umoja wa nchi za Afrika na mpatanishi mkuu katika mazungumzo ya amani ya Sudan kwanza anaelezea nini hasa madhumuni ya mkutano huo.