1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wapalestina wa Gaza waendelea kumiminika Misri

27 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CyP3

JERUSALEM: Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na Rais wa Wapalestina Mahmoud Abbas wamekutana kujadiliana hali ya Ukanda wa Gaza.Mpaka kati ya Misri na eneo la Gaza linalodhibitiwa na chama cha Hamas,bado upo wazi.Wakati huo huo ripoti za vyombo vya habari zinasema,polisi wa Misri wanajitahidi kukagua misafara ya magari lakini watu wanaokwenda kwa miguu wanaendelea kuvuka mpaka bila ya kuzuiliwa.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Wapalestina mjini Ramallah kwenye Ukingo wa Magharibi,serikali hiyo ipo tayari kupeleka vikosi vyake vya usalama kulinda vivuko vya mpakani kwenye Ukanda wa Gaza.Lakini pendekezo hilo limepingwa na chama cha Hamas na hata Israel.Tangu siku 10 zilizopita Israel imefunga vituo vyake vya mpakani vya kuingilia Ukanda wa Gaza kwa sababu ya mashambulizi ya makombora yanayoilenga Israel kutoka eneo la Gaza.