1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanawake mjini Goma, DRC waandamana dhidi ya vita vinavyoendelea kati ya majeshi ya Serikali na Waasi wa CNDP

22 Septemba 2008

Nchini Kongo wanawake wameandamana mjini Goma mashariki ya nchi hiyo wakiwa lengo la kulalamikia vita vinavyoendelea kwenye eneo hilo.

https://p.dw.com/p/FMuy
Wananchi wa Goma wakimbia makazi yao kutokana na vitaPicha: AP

Ghasia zimekuwa zikiendelea kati ya majeshi ya serikali na waasi wa CNDP wanaoongozwa na Jenerali muasi Laurent Nkunda.Mwishoni mwa wiki iliyopita Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Kongo MONUC ulijaribu kupoza mashambulizi yaliyotokea kati ya makundi hayo mawili katika mapigano kwenye eneo la Sake lililo karibu na mji wa Goma.Kwa upande mwingine jana gavana wa mkoa wa Kivu ya Kaskazini Julien Paluku pamoja na waziri wa ulinzi Chikeze Diemo walitekwa nyara na wanawake wawanajeshi kwenyi kambi ya Katindo mjini Goma.

Mwandishi wetu wa Goma John Kanyunyu alishuhudia maandamano hayo na kuandaa taarifa ifuatayo.