1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanariadha mahiri kuiwakilisha Kenya mashindano ya London

28 Juni 2017

Baada ya siku mbili za majaribio katika uwanja wa Nyayo huko Nairobi, Kenya imetangaza kikosi cha wanariadha mahiri kitakachoshiriki mashindano ya dunia yatakayoandaliwa mjini London kati ya Agosti 4 na 13.

https://p.dw.com/p/2fW6R
China Leichtathletik WM in Peking - Männer 1500m - Asbel Kiprop
Picha: Getty Images/A. Lyons

Kikosi hicho kitajumuisha wanariadha sita walioshinda nishani za dhahabu katika makala iliyopita huko Beijing mwaka 2015, ambapo Kenya iliebuka kama timu bora duniani na kuwabwaga miamba wa riadha Marekani na Jamaica. Miongoni mwa wanariadha hao nyota waliotajwa kikosini ni mfalme wa mbio za mita mia nane upande wa wanaume David Rudisha, gwiji wa mbio za kuruka viunzi Hyvin Kiyeng, pamoja na mkongwe Ezekiel Kemboi, mrusha mkuki Julius Yego na Asbel Kiprop.

Nilizungumza na Asbel Kiprop ambaye atakuwa anaingia katika mashindano hayo kama bingwa mtetezi katika kitengo cha mbio za mita 1,500 baada ya kunyakua dhahabu kule Beijing, na kwanza nilimtaka anieleze shabaha ya kikosi cha Kenya safari hii watakapokuwa wakijitosa kwenye mashindano hayo ya dunia.

Mwandishi: Jacob Safari/Reuters/AFPE
Mhariri: Josephat Charo