1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Wanariadha bora wa Kenya watuzwa

11 Desemba 2015

Mabingwa wa dunia Julius Yego na Vivian Cheruyiot wametangazwa kuwa wanamichezo bora mwanamme na mwanamke wa mwaka wa 2015 nchini Kenya

https://p.dw.com/p/1HM84
China Sperrwerfer Julius Yego aus Kenia
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Schiefelbein

Nyota wa mchezo wa kurusha mkuki Yego alipata heshima kubwa kutokana na matokeo yake makubwa katika mashindano ya ubingwa wa dunia mjini Beijing alipokuwa Mkenya wa kwanza kuwahi kushinda taji la dunia katika mchezo huo. Alirusha umbali wa mita 92.72

Cheruyiot, bingwa wa zamani wa ulimwengu katika mbio za mita 10,000 na 5,000 alirejea kwa kishindo na kunyakua taji la mita 10,000 mjini Beijing. Nicholas Bett, aliyeushangaza ulimwengu wakati alipochomoka na kushinda mbio za wanaume za mita 400 kuruka viunzi, alishinda tuzo mbili katika kitengo cha Mafanikio makubwa ya mwaka na mchezaji wa kasi wa mwaka.

Mwanariadha huyo ambaye ni polisi alikuwa Mwafrika wa kwanza kushinda taji la dunia la mita 400 tangu Samuel Matete wa Zambia aliposhinda mnamo mwaka wa 1991 nchini Tokyo.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/Reuters
Mhariri: Iddi Sessanga